Kocha mkuu wa Madini FC, Abdallah Juma amesema kikosi chake kipo tayari kuvaana na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC Jumapili ya wiki hii katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Madini watakuwa wenyeji wa Simba SC katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la ASFC Uwanja wa Sheikh Amri Abedin mjini wakihitaji ushindi kusonga mbele.

Abdalah Juma amesema kikosi chake hakina shaka kuelekea katika mpambano huo dhidi ya Simba na hakuna majeruhi yeyote miongoni mwa wachezaji wake.

Amesema kikosi chake kipo kambini kikijiandaa na mchezo huo, na amewataka mashabiki wa soka wa mkoani Arusha na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya Madini.

kocha Juma amesema anaamini kwa uwezo wa mwenyezi Mungu atashinda pambano hilo, kwani katika mchezo wa soka lolote linaweza kutokea licha ya Simba kuwa timu kubwa na inayoheshimika nchini na barani Afrika.

Kwa upande wao, mashabiki wa soka mkoani Arusha wameonekana kuusubiria kwa hamu kubwa mchezo huo, kutokana na mkoa huo kukosa timu inayoshiriki Ligi

Kuu ya Tanzania Bara kwa takribani miaka mitatu sasa.

Madini ipo Ligi Daraja kwanza Tanzania Bara na ilifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, baada ya kuzifunga JKT Oljoro ya  Arusha, Panone ya Kilimanjaro na JKT Ruvu ya Pwani.

Uwanja Uliolalamikiwa Na Jose Mourinho Wapigwa Kufuli
Yanga Kuifuata Zanaco Bila Ngoma, Tambwe