Hatimaye kilio cha kocha wa Man Utd, Jose Mourinho kuhusu uwanja unaomilikiwa na klabu ya Rostov ya Urusi kimesikika kwa sauti kubwa na kupelekea uwanja huo kufungiwa.

Mourinho aliuponda vikali uwanja huo baada ya timu yake kuminyana na Rostov uwanjani hapo katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Europa, na kushuhudia timu hizo zikipata matokeo ya sare ya 1-1.

Hatua ya kuufungia uwanja huo imechukuliwa na Mamlaka ya Soka ya Urusi ambayo imetoa amri na sharti la kufanyiwa marekebisho ya msingi na kwamba utafunguliwa tena endapo utaonekana kukidhi kiwango cha kimataifa kinachokubalika.

Kilio cha Mourinho na kikosi chake kuhusu uwanja huo ni pamoja na kujaa tope kupita kiasi na baadhi ya maeneo kuwa na vipara, hali inayotengeneza mazingira mabovu ya mchezo husika.

Mawakili wa Manji wawasilisha ‘ombi’ Mahakama isiisome kesi ya ‘Unga’, isikilize ya Uhamiaji
Video: Lissu, Wasonga nusura wazichape kortini, JPM aanza mageuzi kwa sekta ya elimu