Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Singida, SSP. Nestory Didi amewataka abiria kuandika majina sahihi kwenye tiketi zao za kusafiria, ili iwe rahisi kupata taarifa zao kirahisi pindi inapolazimika au kutokea dharula.
Didi, ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva, abiria na watumiaji wengine wa barabara, katika Stendi ya Mabasi ya Wilaya Manyoni.
Aidha, amewataka abiria kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva wa magari wanayopanda, ili wakamatwe na kuchuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kabla ya ajali kutokea.
Hata hivyo, SSP Didi amewasihi Madereva kuuendelea na utii wa sheria za usalama barabarani bila kushurutishwa, kwani jambo hilo ni kwa faida yao na abiria huku akisisitiza matumizi ya kofia ngumu kwa madereva wa pikipiki na abiria wao.