Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amewataka wamiliki wa magari yanayobeba abiria kuwa na leseni ya usafirishaji, sambamba na madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepusha ajali.

Wito huo umetolwa na IGP Sirro Mkoani Iringa, kufuatia kutokea ajali ya basi dogo la abiria Juni 10, 2022 na kuwataka Watanzania uhakikisha wanapewa tiketi wakati wa safari, ambayo ni mkataba kati yao na mmiliki.

“Madereva wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani lakini pia wamiliki wa magari yanayobeba abiria wahakikishe wanakuwa na leseni inayowaruhusua kufanya biashara hiyo,”.

“Wanabeba abiria usiku na bahati mbaya hawatoi tiketi kwa abiria ambazo ni mkataba baina yao, na wanafanya hivi kwa kuwa LATRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu) hawajawapa leseni,” alifafanua IGP Sirro.

Akizungumzia ruhusa ya safari za usiku kwa magari ya abiria, Sirro amesema jeshi hilo linapendekeza baadhi ya njia zitakazoanza usafirishaji kwa majira hayo, hasa katika Mikoa ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.

“Na katika hili tuwe na subira na kama Polisi tumeona kuna hitaji la kusafirisha abiria usiku itakuwa ni kwa baadhi ya njia zenye umuhimu lakini pia niseme yeyote mwenye mashaka ya kutoonekana kwa ndugu yake afike Hospitali kumtabua,” amesema.

Aidha, hapo jana Juni 11, 2022 IGP Sirro pia aliwatembelea majeruhi wa ajali hiyo iliyoua watu 20 katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa wanapopatiwa matibabu baada ya baadhi yao kuhamishiwa hapo kwa matibabu zaidi, ambapo aliwapa pole na kuwafariji.

Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Jasmine Kachela amesema wagonjwa wote wanaendelea vizuri na wanapatiwa matibabu ingawa mmoja kati ya hao yupo Chumba cha Wagonjwa Mahututi ICU.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na Askari katika eneo Changarawe, Mafinga ilipotokea ajali iliyosababisha vifo vya watu 20 Juni 10, 2022,

Mwili wa Padre waokotwa, Polisi ikimsaka mtuhumiwa mauaji
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 12, 2022