Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ACT- Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema katika kusimamia upatikanani wa Zanzibar mpya misingi ya kuwapata viongozi bora kidemokrsia ni lazima ianzie ndani ya chama hicho.

Othman ameyasema hayo akiwa Kwale Jimbo la Ziwani Kisiwani Pemba wakati akizungunza na Viongozi wa Chama hicho katika ngazi za matawi, majimbo Wilaya na Mikoa ya kisiwa cha Pemba.

Amesema, wakati chama hicho kikielekea katika uchaguzi wa ndani ya chama kusijitokeze wanachama kutumia fedha kwani huko ni kujitokeza visuri vya ukiukwaji wa Misingi ya Demokrasi jambo ambalo chama hicho hakitovumilia kuachwa kuendelea jambo kama hilo.

Ameonya kwamba si busara wakati chama kijitayarisha katika kuelekea uchaguzi wa ndani kukajitokeza fitna na majungu kwa viongozi kubeba wagombea jambo ambalo litaharibu misingi ya chama hicho.

Aidha, Othman amabaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amwaeleza viongozi hao kwamba ni jambo la lazima kwa viongozi wa chama hicho kusimamia na kuifuata kikamilifu misingi ya uongozi bora katika safari ya ujenzi wa Zanzibar mpya yenye malengo ya kusimamia demokrasi ya kweli nchini.

Bruno Gomez mambo magumu Simba SC
Mwigulu: Simba SC ifuate nyayo za Young Africans