Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Adam Lallana amekubali kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu kwa kandarasi maalumu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 32, angeondoka huru mwishoni mwa mwezi Juni ambapo ndio tamati ya mkataba wake wa sasa, lakini mkataba mpya utaendelea kumpa fursa ya akisalia klabuni hapo.
Msimu wa 2019-20 utaendelea Juni 17 baada ya mapumziko ya zaidi ya siku 100 kutokana na uwepo wa janga la virusi vya Corona.
“Hii ina maana kubwa kwenye maisha yangu, nafasi niliyopewa niyakipekee kwangu na familia yangu pia”. Amesema Lallana
“Siku zote nimekuwa nikifikiria kufanya jambo njema kwa klabu” Ameongeza.
Liverpool wanaongoza msimamo wa ligi kuu nchini England kwa tofauti ya alama 25 kwa timu iliyonafasi ya pili Manchester City, kama watafanikiwa kuchukua taji itakuwa mara ya kwanza baada ya miaka 30.
Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Everton Juni 21 wakati ya mwisho itakuwa dhidi ya Newcastle United Julai 26.
Lallana alijiunga na Liverpool mwaka 2014 akitokea Southampton ambapo alisajiliwa na aliyekuwa kocha mkuu Brendan Rodgers ambapo hivi sasa anahusishwa kujiunga nae tena Leicester City.