Mshambuliaji wa Young Africans David Molinga “Falcao” amekacha safari ya mkoani Shinyanga kwenye mchezo wa ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC ambao utapigwa Uwanja wa CCM Kambarage siku ya Jumamosi.

Molinga ni miongoni mwa wachezaji ambao walipaswa kuondoka Alfajiri ya leo, lakini mshmbuliaji huyo kutoka DR Congo ameingia mitini kwa kile alichoeleza kuwa jina lake halikuwemo kwenye orodha iliyotangazwa na kocha Msaidizi Charles Mkwasa jana jioni.

“Nataka nikanushe hii habari kwamba nimegoma kusafiri na timu. kwanza nimewakumbushe kitu cha peke imenileta Tanzania ni mpira na kazi yangu ndio iyo.”

“Sasa iko ivi tangu timu imeanza mazoezi sijawahi kukosa na nafata program za Mwalim vizuri lakin jana list ilitoka na mimi jina langu ajakwepo sasa itasemekana vipi mimi nimegoma?”

“Kama ndio ivyo muulizeni coach ndio alitajia list yake. imekuwa tabia kila mara kila kitu mimi tu ata kama sijafanya kitu kibaya utaskia tu Molinga this is too much,” aliandika Molinga kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Hii sio mara ya kwanza kwa Molinga na Young Africans kuingia kwenye mvutano hasa pale timu inaposafiri kwenda kucheza mikoani.

Mchezo wa mwisho dhidi ya Namungo FC kabla ya ligi kusimama kutokana na janga la Corona, Molinga aligomea safari ya mkoani Lindi akitoa udhuru kuwa mkewe ni mgonjwa.

Nyota huyo ameingia kwenye migogoro ya mara kwa mara na uongozi wa Young Africans.

Adam Lallana mambo safi Liverpool
Mo Dewji awatuliza Simba SC