Waimbaji mahiri wa muziki kutoka Uingereza Ed Sheeran na Adele wapemeutupilia mbali mualiko wa kutumbuiza kwenye hafla ya baada ya kutawazwa kwa Mfalme Charles wa tatu, ifikapo Mei 7, 2023.
Taarifa za awali kutoka kwa mmoja wa waandaji wa tukio hilo inadaiwa kuwa Mfalme Charles ndiye aliyependekeza majina mawili ya nyota hao, miongoni mwa orodha ya washereheshaji muhimu walichaguliwa kwa ajili ya hafla hiyo.
Inaelezwa kuwa ilipofika wakati wa kuanza kupangwa kwa tukio la kutawazwa kwa Mfalme Charles Mei 6 – na tamasha litakaloambatana na wikendi ya sherehe siku ilitakayofuata, Mei 7, Charles tayari alikuwa na waimbaji wawili aliopenda wahudhurie hafla hiyo kwenye orodha yake ya lazima.
“Mfalme amependekeza watu kadhaa ambao angependa wahudhurie kama sehemu ya washereheshaji, na Adele na Ed walikuwa kwenye orodha hiyo. Alikuwa na hamu sana kwamba wangekuwa sehemu ya tamasha hilo.” amesema mmoja wa waratibu wa hafla hiyo.
Kwa mujibu wa OK, nyota hao wawili wote wamedaiwa kukataa muwaliko wa kutumbuiza kwenye tamasha hilo. kwa upande wa Ed Sheeran yeye amewasilisha majibu yakukataa mualiko huo kwa madai ya kuwa siku hiyo atakuwa kwenye onyesho lingine siku moja kabla ya hafla hiyo ya King Charles, hivyo kufanya iwe vigumu kufika. Lakini kwa upande wa Adele, inaelezwea kuwa yeye “alikataa mwaliko huo bila maelezo.”
“Kuna timu iliyoundwa ili kuhakikisha inawapata watu mashuhuri waliotakiwa kwenye hafla hi waliwasiliana na wawili hao, lakini wakapata majibu wakisema hawapatikani, jambo ambalo lilikatisha tamaa sana,” chanzo kilisema. “Wao ni wakuu wa tasnia ya showbiz na ni Waingereza kabisa, lakini pia wanajulikana kote ulimwenguni. kukataa kwao licha kuwa na shughuli nyingine ila ni aibu sana.”
Pamoja na mgogoro huo kuhusu Adele na Ed Sheeran, Wengine wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye hafla hiyo ni pamoja na Lionel Richie na Spice Girls, huku kukenea tetesi za kuwa Harry Styles pia anaweza kupanda jukwaani.