Waziri wa Maji, Jumaa Aweso yupo jijini London, Uingereza kuhudhuria Mkutano maalum wa sekta ya Maji Duniani (World Water Innovation Summit (WWIS) 2023), ambapo pia alipata wasaa wa kuzungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Waziri Aweso ambaye amembatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wamewasili London Mara baada ya kuwasili jijini humo, pia alisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro wakiwa na ujumbe na watendaji wa ubalozi.

Kupitia Mkutano huo unaohusisha wadau wa sekta ya Maji duniani, Viongozi na wataalamu watajadili changamoto zinazoikabili sekta katika mifumo ya usambazaji maji na usafi wa mazingira (majitaka).

Aidha, Mkutano huo unatarajiwa kuwa na mjadala wenye kutoa suluhu ya pamoja ya namna bora ya kuboresha mifumo ya usambazaji Majisafi na usafi wa mazingira na utekelezaji wa Miradi mikubwa ikiwemo ya mabwawa inayoendelea na inayotarajiwa kujengwa nchini.

Azam FC yatuma salamu nzito Msimbazi
Adele na Ed Sheeran wampiga chini king Charles III