Mtoto wa Mama mjamzito ambaye alikuwa amenasa chini ya jengo lililoporomoka huko Aleppo, Syria baada ya tetemeko la ardhi aliyejifungua chini ya kifusi na kufariki kabla ya waokoaji kumfikia, anaendelea vizuri.
Tukio hilo la kushangaza, lilijiri saa chache baada ya shirika la kujitolea la Syria kuchapisha video inayoonyesha mtoto mdogo akitolewa akiwa hai, kutoka kwenye vifusi vya tetemeko la ardhi katika kijiji cha Qatma.
Vifo katika Syria na Uturuki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi la 7.8 za kipimo cha richa imefikiwa watu 7,200 huku Shirika la Afya Ulimwenguni WHO likisisitiza uokoaji wa watu waliokwama kwenye vifusi katika hali ya baridi uendane na muda.
Aidha, waokoaji wamesema walisikia sauti ya mtoto na walichimba wakamkuta mtoto huyo huku kitovu chake kikiwa bado kimeungana na cha mama yake ambapo baba na ndugu zake wengine wanne wa kuzaliwa naye, wakikutwa wamefariki kutokana na tetemeko hilo.