Mtu mmoja, Michael Mwambaja anashikiliwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa tuhuma za kuua Twiga na kuchoma nyama yake aliyokuwa amepanga kwenda kuiuza.

Mtuhumiwa, Michael Mwambaja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema limetokea usiku wa kuamkia Februari 7, 2023 katika kijiji cha Madundasi kinachopakana Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Nyama ya Tiga iliyokuwa ikichomwa kwa ajili ya kupelekwa sokoni.

Amesema, kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na msako uliofanywa na askari hao wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambao bado wanamsaka mtu mwingine anayedaiwa kushirikiana na Mwambaja.

Ngozi ya Mnyama aliyeuawa na Mwambaja.

Mtuhumiwa huyo (Mwambaja), pia alipatikana akiwa vitu mbalimbali ikiwemo dawa za asili ambazo humsaidia asionekane na askari na pia wanyama wasiweze kukimbia.

Vifaa alivyokutwa navyo Mwambaja vikitekezwa.

Try Again uso kwa macho na Infantino
Waandamana kupinga marekebisho ya umri wa kustaafu