Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amekutana na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ Gianni Infantino katika Kozi ya Diploma ya Uendeshaji wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika nchini Morocco.

Try Again ni miongoni mwa viongozi wachache wa klabu Afrika waliopata nafasi ya kushiriki kozi hiyo, ambayo moja ya waendashaji ni Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger.

Try Again amesema kozi hiyo itaisaidia Simba SC kuboresha uendeshaji wa Klabu na itakuwa mfano kwa timu nyingine katika mambo mengi.

“Hii ni fursa kubwa ambayo tumeipata Simba SC, itatusaidia kuboresha uendeshaji wa klabu. Tutakuwa timu bora ambayo itakuwa mfano kwa nyingine,” amesema Try Again.

Try Again amesema wakati kozi inaendelea, FIFA na CAF wanaendelea na mipango ya maandalizi ya Super Cup ambayo Simba SC itashiriki Michuano hiyo.

Young Africans yaondoka Dubai
Jangili Ruaha atiwa nguvuni