Wawakilishi Pekee wa Tanzania kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi Simba SC, wamesisitiza kupambana Kufa na Kupona, watakapocheza ugenini dhidi ya Horoya AC mwishoni mwa juma hili (Jumamosi Februari 11).

Simba SC itakua mgeni wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa General Lansana Conte mjini Counakry, saa kumi kwa majira ya nchini Guinea.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu hiyo ya Msimbazi Ahmed Ally amesema, mipango mikubwa ya Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha Roberto Oliveira, ni kuona kikosi chao kinapambana na kupata ushindi ugenini.

Ahmed amesema Kocha huyo amekua akiwasisitiza wachezaji wake kuhakikisha hilo linafanikiwa, na kama mambo yatakuwa magumu basi wanapaswa angalau kupata matokeo ya sare ambayo yatakuwa mazuri kwa upande wao.

“Mpango wetu wa kwanza kule Guinea ni kuhakikisha tunapata ushindi. Kama mambo yatakuwa magumu basi tusifungwe na tusishinde.”

“Kiujumla maandalizi mengine ya mchezo wetu wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Horoya AC yanakwenda vizuri.” amesema Ahmed Ally

Kuhusu mipango yao watakapofika nchini Guinea, Ahmed amesema tayari Uongozi wa Simba SC umewatanguliza baadhi ya maafisa wake, ambao wanafanya kazi kubwa itakayosaidia kikosi chao kuishi kwa amani na utulivu kwa muda wote watakaoishi mjini Counakry

“Tumeshatanguliza watu Guinea kwa ajili ya Logistics mbalimbali.” ameongeza ahmed Ally

Wakati Simba SC ikitarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kundi C Jumamosi (Februari 11), Mabingwa wa Soka nchini Morocco Raja Casablanca wataikaribisha Vipers SC mjini Casablanca kwenye Uwanja wa Mfalme Mohammed V Ijumaa (Februari 10), kuanzia saa mbili usiku kwa majira ya Morocco.

Uteuzi: Wanane wateuliwa ujumbe wa Bodi TAFORI
Zaidi ya mil. 710 zatumika ujenzi kitovu cha utalii