Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kimeondoka Dubai mapema leo Jumatano (Februari 08) majira ya asubuhi kuelekea Tunis-Tunisia.

Young Africans ilianza safari jana Jumanne (Februari 07) majira ya Mchana ikitokea Dar es salaam kupitia Dubai kwa usafiri wa Ndege ya Shirika la Ndege la Fly Emirates.

Kikosi cha Young Africans kikiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai kabla ya kuendelea na safari ya Tunis-Tunisia.

Kwa mujibu wa Kurasa za Mitandao ya kijamii za Young Africans, Kikosi cha Wachezaji, Maafisa wa Benchi la Ufundi na Baadhi ya viongozi wameonekana wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.

“Safari ya kuondoka Dubai kuelekea Tunisia imeanza ✈️” imeandikwa kwenye kurasa za Mitandao ya Kijamii za Young Africans.

Wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23, watacheza dhidi ya US Monastir ya Tunisia Jumapili (Februari 12), katika Uwanja wa Hammadi Agrebi, mjini Tunis.

Ahmed Ally: CAF imetupa masharti maalum
Try Again uso kwa macho na Infantino