Taasisi ya Blue Carbon UAE na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wametia saini Mkataba wa Makubaliano kuanza kwa ushirikiano wenye lengo la kukuza usimamizi endelevu wa misitu na kupunguza ukame.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema biashara ya kaboni itasaidia kuleta fursa nyingi hapa nchini kuhifadhi mazingira katika hafla na Mwanamfalme wa Dubai ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon, Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum na Waziri Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana.

Kamishna Mkuu wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Pro. Dos Santos Silayo (kulia) na Bi. Josiane Sadaka wakisaini hati za makubaliano kuhusu biashara ya kaboni kwa niaba ya TFS na kampuni ya Blue Carbon katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu jijini Dodoma leo Februari 06, 2023.

Amesema, hii ni mara ya kwanza kwa makubaliano hayo baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha uandaaji wa kanuni na mwongozo wa biashara ya kabini Oktoba 2022 na hatua hiyo itafungua milango kwa wananchi kupanda miti kwa wingi na kutunza mazingira, ili iweze kuingia kwenye biashara hiyo.

“Ni Imani yetu sasa tutategemea kuwa na fursa nyingi pamoja na kurudisha hali ya mazingira iliyoharibika na tunaona hata mikoko pia inaingia katika baishara ya kaboni hivyo TFS sasa watakuwa na uwanja mpana wa kuhakikisha misitu yetu inahifadhiwa,” amesema Jafo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt, Pindi Chana naviongozi mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanamfalme wa Dubai ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon, Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum na ujumbe wake mara baada ya hafla ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano kati ya kampuni hiyo na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuhusu biashara ya kaboni, leo February 06, 2023.

Kwa upande wake, Mwanamfalme, Sheikh Al Maktoum akiwa na ujumbe wake amesema ushirikiano huo utajikita katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi, kusimamia na kusajili rasilimali zake za misitu.

Hifadhi hizo zenye ukubwa wa hekta milioni 8 katika awamu ya kwanza ya kwanza ikijumuisha hekta 56,000 za mikoko chini ya kifungu cha 6 cha Mkataba wa Paris hivyo kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, katika kuendeleza miradi mipya ya kukabiliana na kaboni.

Bishara ya Kaboni: Watanzania wahimizwa kupanda miti
Maboresho ya Elimu: GGML yakabidhi madarasa Shule ya msingi