Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa Godfrend Brown (44), mkazi wa Sanya Juu mkoani Kilimanjaro na Stive Haule (32), dereva wa lori na mkazi wa Moshi wakiwa na pombe za bandia boksi 154, vifaa mbalimbali vya kutengeneza kinywaji hicho, stika mbalimbali za makampuni ya vinywaji na vifungashio vya pombe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Kamishina msadizi wa Polisi Justine Masejo aliyoitoa hii leo Februari 6, 2023 Mkoani humo, imesema operesheni hiyo iliyohusisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kata ya Moivo, iliyopo tarafa ya King’ori Wilayani Arumeru.

Vifaa vilivyoakatwa ambavyo hutumika kutengenezea Pombe bandia.

Amesema, mtuhumiwa Stive Haule alikamatwa akiwa na gari aina ya Scania lenye namba za usajili T191 CTB lenye tela la namba za usajili T823 DHC likiwa na ujazo wa lita 35,000 za spiriti wakati likiwa linashusha mzigo wa spiriti kwa lengo la kwenda kutengeneza pombe bandia.

Aidha, Uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo vya kihalifu kwa muda mrefu na upelelezi ukikamilika, jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kulitolea uamuzi wa kisheria.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 7, 2023
Ntibazonkiza alamba kitita Simba SC