Afrika Kusini imetangaza kwamba itafungua mipake yake ili kuruhusu wageni kutoka mataifa mbalimbali kuingia nchini humo na kuwezesha raia wake kusafiri nje ya nchi ifikapo OKtoba 1.
Akilihutubia taifa kwa njia ya televishenio Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema orodha sahihi ya nchi zinazohusika na vizuizi vilivyowekwa na mamlaka nchini humo itatolewa baadaye kulingana na taarifa za hivi karibuni za kisayansi.
Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize amesema utafiti wa wataalamu wa afya nchini humo umebaini kuwa, watu milioni 12 ambao ni sawa na asilimia 20% ya idadi ya watu nchini humo, huenda tayari wameambukizwa virusi hivyo, katika nchi hiyo ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Sita.
Utafiti huo unaonesha kuwa idadi halisi ya maambukizi inaweza kuwa kubwa zaidi, kati ya 35% na 40%, na watu waliothirika zaidi ni wale wanaishi katika maeneo ambayo kuna watu wengi.
Afrika Kusini ilifunga mipaka yake Machi 27 mwaka huu kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona na mwezi Julai, kati ya kesi mpya 10,000 na 15,000 ziliripotiwa kila siku,lakini katika siku moja iliyopita, kesi mpya 956 tu ndizo zilizoripotiwa.