Mahakama ya Wilaya ya Serengeti imemuhukumu mkazi wa kijiji cha Nyakomogo, Joma Masoya (34) kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na vipande vinne vya nyumbu.

Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Serengeti Judith Semkiwa amesema kuwa kosa la kuingia kwenye hifadhi bila kibali adhabu yake ni mwaka mmoja, kukutwa na silaha hifadhini adhabu yake ni miaka miwili na kukutwa na nyara za Taifa adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 gerezani.


Hukumu ya kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 55/2020 iliyosomwa leo Julai 30, 2021 na Hakimu Mkazi wa Wilaya, Semkiwa ambapo mshtakiwa ametiwa hatiani kwa makosa matatu aliyoshitakiwa nayo.

Aidha mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Jakobo Matatala ameiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alikamatwa Julai 12, 2020 katika milima ya Kirawila ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kinyume na sheria.


Alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kuingia hifadhini bila kibali, kukutwa na silaha za jadi hifadhini bila kibali na kukutwa na vipande vinne ambavyo ni sawa na nyumbu mzima bila kibali na kuomba mahakama kutoa adhabu kali.

Mashitaka hayo yamempelekea kuhukumiwa ambapo Mshitakiwa ameomba apunguziwe adhabu kwa kuwa anategemewa na familia.

Chanjo ya Uviko 19 kutolewa bure
Rais Samia apokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Tshisekedi wa DR Congo