Baadhi ya Wanawake wamekuwa wakishuhudia kupoteza hamu ya tendo la ndoa baada ya kutumia uzazi wa mpango na kupelekea migogoro ya kimahusiano kwa wenzi wao.

Hali hiyo, imesababisha mahusiano au ndoa nyingi kupoteza mvuto au kuvunjika kabisa baada ya kuibuka kwa ugomvi baina yao, ukihusisha wivu na hisia mbaya pale inapotokea mmoja wao hakubali sababu husika ya mwenzi wake.

Lakini wengi hawatambui kuwa uzazi wa mpango hasa unaotumia hormones za kutengenezwa hupelekea kuvurugika kwa mfumo wa asili wa hormones katika mwili hasa zile hormones zinazochochea hamu ya tendo la ndoa.

Wataalamu wa masuala ya Afya wamekuwa wakisema kwamba uzazi wa mpango unazuia uzalishaji wa hormones zinazosaidia kuongezeka kwa hormones za mapenzi mwilini ndiyo maana mtu anakosa hamu Ya teno la ndoa.

Sasa vipo vyakula ambavyo husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa na mvuto kwa mwenzi wako ikiwemo Chocolate hasa ile nyeusi inatajwa kusaidia mzunguko wa damu vizuri hasa kwenye via vya uzazi vya mwanamke na kuongeza hisia za tendo la ndoa.

Aidha, mbegu za maboga nazo pia husaidia kuzalishwa kwa hormones za kuchochea hamu ya tendo la ndoa kwa kiasi kikubwa na kuongeza hisia bila kusahau Kitunguu saumu ambacho nachi ni tiba ya mzunguko wa damu hasa katika via vya uzazi.

Tunda la Nanasi pia husaidia kuongeza hisia wakati wa tendo, hasa kile kiini cha katikati na Tangawizi ambayo nayo imejumuishwa katika kusaidia kuongeza mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi na kuongeza hisia wakati wa tendo la ndoa.

Mboga ya majani aina ya Spinach ni nzuri kwa afya ya uzazi ya mwanamke, inatajwa kusaidia kuongeza hisia wakati wa tendo, na pia huongeza mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi kama ilivyo kwa Strawberries ambayo nayo huzalisha hormones za kuchochea hamu ya mapenzi na Parachichi ambalo huongeza nguvu mwilini na kuleta hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke.

Majimengi kukabidhiwa Gwanda Namungo FC
Minziro anataka wawili Tanzania Prisons