Afisa afya kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Jackline Saulo amesema elimu ya kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko ni muhimu na kwamba watumishi wa afya ngazi ya Jamii wana umuhimu mkubwa wa kuhakikisha wanafikisha elimu ya afya katika maeneo yao.

Saulo ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi katika kituo cha afya cha Kimeya Wilayani Muleba, mara baada ya timu ya wataalam wa afya kutoka Mkoa wa Kagera na Halmashauri ya Muleba kujionea kanuni za afya za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko zinavyozingatiwa na kituo hicho.

Amesema, “sasa hivi tunaendelea kutembelea katika jamii ,vituo vya kutolea huduma ya afya,wagonjwa wote wanaotufikia tunatakiwa kuwafikishia elimu ya kutosha namna gani ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.”

Awali, Kaimu Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya cha Kimeya Dkt. Albert Bongo alisema baada ya mlipuko wa ugonjwa wa Marburg, hatua mbalimbali za afya zilichukuliwa kituoni hapo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uwepo wa vifaa vyote vya usafi na watalaam wa afya kujengewa uwezo.

Akitoa elimu ya afya kwa watu waliofika katika kituo hicho kupata huduma za matibabu, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma Halmashauri ya Muleba, Johanes Mutoka alisema ni muhimu kuacha tabia ya kusalimiana kwa kushikana mikono, ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Fei Toto kuvaa medali Ligi Kuu, ASFC, CAF
Dante: KMC FC tunazitaka alama sita ugenini