Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Festo Dugange amewaagiza waganga wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha kuwa wanasimamia watendaji wa vituo vya kutolea huduma za afya kuweka kumbukumbu za dawa, vifaa tiba, vitendanishi vinavyonunuliwa pamoja na mapato yatokanayo na huduma hizo

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya Mvomero mara baada ya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo kushindwa kueleza kumbukumbu za dawa, vifaa tiba, vitendanishi pamoja na mapato ya hospitali hiyo licha ya hospitali hiyo kuwa na dawa zote muhimu zinazohitajika.

Amesema serikali haipo tayari kuona mali inazonunua zinapokelewa na zinatumika bila kuwa na kumbukumbu zinazotakiwa.

“Tukifika katika kituo tukute mtiririko wote wa kumbukumbu zote umeainishwa, wahusika wamesaini, na hizo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinaonekana na kama vimetumika tunajua nani ametumia.

Amesema serikali inapotaka kununua dawa asihusike mtu mmoja peke yake maamuzi ya dawa zipi zinunuliwe, za shilingi ngapi, zinanunuliwa wapi, maamuzi yafanywe na kamati ya matibabu ya kituo ambayo ina wajumbe kadhaa, ambao watasaini na kukubaliana kuwa inakwenda kununua dawa hizi.

Amesisistiza dawa hizo ziingizwe kwenye leja na zinapotoka bohari kuu ziende kwenye bohari ndogo na kwenda kwa mgonjwa ili kila sehemu nani alizitoa hapa na kuzipeleka dispensing, akapeleka kwa wagonjwa nani ni mgonjwa gani alipata zile dawa.

“Bado sijaridhishwa na ufanisi wa makusanyo ya huduma za uchangiaji. Mganga mfawidhi hujui kwa siku anakusanya shilingi ngapi, katika seksheni ipi tunachotaka kila sehemu ijipime, maabara ijipime wao wanachangia kiasi gani kwa siku, kwa mwezi na kwa mwaka, dawa wajipime, wodi ya watoto wajipime, kwa sababu hivyo vyote ndiyo vyanzo vya huduma, lakini pia ndiyo vyanzo vya mapato” amesema Dkt. Dugange

Dkt. Dugange amesema hatarajii kuona hakina kumbukumbu ya dawa, vitendanishi na vifaa tiba pamoja namapato ya kituo husika.

Kardinali Pengo umelifanya Jimbo la Mpanda kujitegemea -Askofu Nzigirwa
Aharibu mazao ya Sh4 Milioni, baada ya mkewe kukataa kupumzika ‘Siku ya Baba Duniani’