Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema hakuna njia ya mkato kwa kikosi chao zaidi ya kuhakikisha kinabadilika na kushinda michezoya ugenini, ili kutimiza lengo la kuwania ubingwa msimu huu 2022/23.

Simba SC ilipata sare ya nne msimu huu juzi Jumatano (Novemba 23) dhidi ya Mbeya City iliyokua nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, ikitanguliwana sare dhidi ya Singida Big Stars, Young Africans na KMC FC huku ikipoteza kwa Azam FC.

Ahmed Ally amesema endapo kikosi chao kitaendelea kuangusha alama katika michezo ya ugenini, mambo yataendelea kwenda kombo na Ubingwa watausikia kwenye ‘Bomba’.

“Kama hatuwezi kushinda michezo ya mikoani ‘Ugenini’ tunajiweka katika mazingira magumu ya kushinda ubingwa. Kama tutakuwa na muendelezo huu wa matokeo hayo ya mkoani unauweka ubingwa Rehani.” amesema Ahmed Ally

Katika hatua nyingine Ahmed Ally amesema Simba SC inakabiliwa na changamoto ya kushindwa kuwatumia ipasavyo Wachezaji wake wa Kimataifa ambao walisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu, kwa ajili ya kuisaidia timu kupambana ndani na nje ya nchi.

Amesema hadi sasa Simba SC imekua ikinufaika na mchango wa wachezaji wawili pekee wa Kimataifa (Okrah na Phiri), ambao wanatumika mara kwa mara, lakini wengine wamekua wakisuasua, hivyo kuna ulazima kwao kama viongozi kutatua tatizo hilo.

“Msimu huu tulisajili wachezaji 7, lakini wachezaji wawili ndiyo wameingia kikosi cha kwanza (Okrah na Phiri) ukitazama wengine bado wanasuasua. Hivyo dirisha dogo kuna haja ya kurudi sokoni kuleta vyuma vingine. Timu yetu ya sasa haijafikia ‘levo’ ambayo Wanasimba tunaihitaji” amesema

M23: Hatutambui wito kikao cha Angola
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 25, 2022