Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally, amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa msimu mpya wa 2023/24.

Mastaa wa Simba SC ikiwa ni pamoja na Luis Miquissone, Clatous Chama, Fabrice Ngoma, Kibu Dennis, John Bocco wameweka kambi Uturuki ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.

Ni Agosti Mosi msafara wa kikosi cha Simba SC unatarajiwa kuwasili Bongo baada ya kambi ya muda iliyoanza Julai 12 huku wakiwa wanaelekea kwenye Simba Day, Agosti 6.

Akizungumza jijini Dar es salaam Ahmed Ally amesema kuwa, wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na watatoa burudani kubwa kila mchezo.

“Wachezaji wa mpira wote wapo fiti kwa msimu mpya na juhudi wanazoonyesha kwenye maandalizi ni picha kubwa kuelekea kwenye ushindani mpya ndani ya msimu mpya.

“Ukianza na Luis, Kibu Dennis, Chama hawa wote wanafanya vitu vikubwa na vizuri kwenye mazoezi hilo linatupa nguvu ya kuamini kwamba tunakwenda kwenye ushindani mkubwa tukiwa na wachezaji imara.

“Kwa msimu mpya tunakwenda kuanza kwa mtindo mpya wa kusaka ushindi kila mechi huku tukiwapa burudani mashabiki hilo linakwenda kudhihirika Simba Day kisha kwenye mechi zinazofuata,” amesema Ahmed Ally

Wakulima ongezeni thamani ya zao la Alizeti - COSITA
Hospitali ya Muhimbili yapitishwa CAF