Meneja wa Habari na Mawasilino wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ahmed Ally ameonesha kukerwa na baadhi ya Mashabiki wa Young Africans waliojitokeza kuiopokea RS Berkane walipowasili Dar es salaam jana Alhamis (Machi 09).

Ahemd ameonesha kukerwa huko kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram, huku akiwasili baadhi ya mashabiki hao wa Young Africans kuwapitisha kila mahala wageni wao.

Ahmed Ally ameandika: Mashabiki MSETO asanteni kwa kuwapokea wageni wetu…Tunathamini juhudi zenu??

Kesho (LEO) msisahau kuwaonesha msikiti wapate Ijumaa na baada ya hapo wapelekeni kwenye Biriani si mmeamua na nyie mjitafutie shughuli ya kufanya kwenye WIKI YA WAKUBWA

Any way sisi tunaendelea na mazoezi yetu na tupo tayari kwa Jumapili

Insh Allah ???? tutacheka mwisho

Simba SC ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane katika mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa Kundi D, Februari 27 mjini Berkane-Morocco hivyo itahitaji kulipa kisasi kwa kusaka ushindi ili kurejea kileleni mwa msimamo wa Kundi hilo.

Kabla ya mchezo huo Simba SC ilikua inaongoza msimamo wa Kundi D kwa kuwa na alama 04, huku Berkane iliyopoteza mchezo wa Mzunguuko wa pili dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ilikua na alama 03.

Hadi sasa Msimamo wa Kundi D, unaonyesha kuwa RS Berkane inaongoza ikiwa na alama 06, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama o4 sawa na USGN ya Niger huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast ikiburuza mkia ikiwa na alama 03.

Balozi Mulamula atembelea ofisi za ubalozi jijini RIYADH
Madini ya magari ya Umeme kuanza kuchimbwa Tanzania