Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally ni kama amejibu kauli za Wadau wa Soka ambao walionesha kushagazwa na maamuzi ya Uongozi wa Klabu hiyo kutangaza kuachana na Kiungo Jonas Gerard Mkude.

Simba SC ilitoa taarifa za kuachana na Kiungo huyo aliyedumu kwa miaka 13 klabu hapo Juni 23, 2023 baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuandika mipango ya Uongozi wa Simba SC iliyoandaliwa kwa ajili ya Jonas Mkude ambaye alionekana kama ameachwa kwa kutopewa heshima yake ndani ya klabu hiyo.

Ahmed Ally ameandika: Muda umetenganisha mapenzi yetu na Jonas Mkude

Ameondoka mtu tunaempenda kweli, ameondoka Mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu

Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda

Wakati Simba ina njaa, Azam ilimhitaji hakuenda, UTO walimtaka hakuenda akachagua kuvumilia njaa yetu huyu ni zaidi ya mchezaji kwetu

Sisi tulitamani Jonas Mkude amalizie mpira wake Simba kwani hatutaki kucheza nae akiwa timu nyingine

Kwa sababu tukimfunga ataumia na yeye akitufunga ataumia hatuko tayari kumuumiza Mkude wetu

Tumetoa taarifa ya kuachana nae punde tutatoa taarifa ya kumuaga na tutamuaga kwa heshima zote

Sisi ndo tunatambua zaidi heshima ya Mkude kuliko mtu mwingine yeyote na tutamuaga kwa heshima hiyo hiyo

Kila la heri Legend @jonasmkude20

Wananchi: Waziri Mwigulu amekurupuka, hatushirikishwi
Josko Gvardiol anawindwa mitaa ya Manchester