Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewataka wanachama na mashabiki wa Klabu hiyo kufunga mjadala wa uchaguzi uliofanyika jana Jumapili (Januari 29).
Uchaguzi wa viongozi Simba SC ulitanguliwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Ahmed Ally ametumia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuwasihi Wanachama na Mashabiki wa Simba SC kufunga ukurasa wa Uchaguzi Mkuu na badala yake wawaunge mkono wale wote waliochaguliwa kwa maslahi ya klabu yao.
“Jukumu letu ni kuwaunga mkono kwa maslahi ya Simba, tukiwadhoofisha tumedhoofisha Simba tukiwapa nguvu tumeipa nguvu Simba” ameandika Ahmed kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Hatuna muda tena wa kuendelea na mjadala wa uchaguzi, sasa tunarejea kwenye jukumu letu la msingi kucheza mpira” ameongoza Ahmed
Katika uchaguzi huo ambao matokeo yake yametangazwa leo Jumatatu (Januari 30) Afajiri, Kaluwa amepata kura 1,045 huku Mangungu ambaye alikuwa anatetea kiti chake akipata jumla ya kura 1,311.
Kwa upande wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walioshinda ni Dr Seif Ramadhan Muba (1636), Asha Baraka (1564), CPA Issa Masoud Iddi (1285), Rodney Chiduo (1267) na Seleman Harubu (1250).
Jumla ya Wanachama Simba SC waliopiga Kura ni 2363 Kura halali, lakini Kura halali zilikuwa 2356.