Beki wa pembeni wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles atakua nje ya uwnaja kwa kipindi cha majuma sita, baada ya kuthibitika amepata mpasuko katika mpupa wa mguu wake wa kushoto.
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Arsenal leo mchana imeeleza kuwa, beki huyo mwenye umri wa miaka 20, amebainika kuwa ma mpasuko mdogo kwenye mfupa wa fibula, baada ya kupata majeraha akiwa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huu wa 2018/19 mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Manchester City, waliochimoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Wakati beki huyo akiwa katika matarajio ya kurejea tena uwanjani baada ya majuma sita, beki mwenzake Carl Jenkinson hatocheza mpira kwa kipindi cha majuma sita hadi manane kufuatia majeraha ya kifunzo cha mguu, huku Nacho Monreal akirejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza.
Beki mwingine Sead Kolasinac anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi Oktoba, baada ya kuumia katika michezo ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi ya England.
Arsenal wanaendelea na maandalizi ya mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi kuu ambao utachezwa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge.