Rasmi Mlinda Lango chaguo la Kwanza Simba SC Aishi Manula, atakosa sehemu ya msimu iliyosalia, kufuatia majeraha ya bega aliyoyapata kwenye mchezo wa Robo Fainali, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Ihefu FC.

Tayari Manula amekosa michezo mitatu ya Ligi Kuu dhidi ya (Ihefu FC, Young Africans na Namungu FC) na mwili ya LIgi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad AC (nyumbani na ugenini) kutokana na majeraha hayo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally, Mlinda Lango huyo ataendelea kuikosa michezo yote ilizosalia katika Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

“Wachezaji wote ni wazima na wanajiandaa na mchezo wa Jumapili dhidi ya Azam FC, lakini Manula na Mohammed Ouatarra, hawatokuwa sehemu ya michezo yote iliyosalia,” amesema.

Katika Ligi Kuu Bara, Simba SC imebakisha michezo mitatu dhidi ya Ruvu Shooting, Polisi Tanzania na Coastal Union.

Manula Aliyeichezea Simba kwa mafanikio, amedumu kwa miaka sita, alitua klabuni hapo mwezi Agosti mwaka 2017, akitokea Azam FC.

Watumishi wa Serikali wakumbushwa uzingatiaji wa maadili
Adha ya Barabara Kashai: CCM yatoa maagizo kwa Mkandarasi