Takriban Watu 13 wamefariki na wengine 32 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria Kampuni ya Ally’s Star lenye namba za usajili T 178 DVB, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha treni kilichokuwa kikisafiri kutoka Itigi kuelekea Manyoni Mkoani Singida.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Stella Mutabihirwa amesema ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Novemba 29, 2023 na majeruhi wamepelekwa katika hospitali za Itigi na Manyoni kwa ajili ya matibabu huku Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni Dkt. Furaha Mwakafira akikiri kupokea miili ya watu 13 na majeruhi hao.