Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limewakamata watuhumiwa 107 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya Mauaji, Wizi ya Mifugo, Unyang’anyi wa kutumia silaha, kuingia nchini bila kibali pamoja na kupatikana Dawa za kulevya, huku watuhumiwa 41 wakifikishwa Mahakamani, kesi 11 zikiendelea na nyingine zikitolewa hukumu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi, Almachius Mchunguzi amesema kati ya watuhumiwa hao 21 wamekamatwa na Bangi kilogramu 43, Mirungi Kilogramu 124, Heroin Gramu 242 huku wanne wakikamatwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu na watuhumiwa saba raia wa Ethiopia kuingia nchini bila kibali.

Amesema, katika kuimarisha doria za nchi kavu na Baharini, Novemba 21, 2023 maeneo ya Kisiwa cha Jambe Wilaya ya Tanga, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata boti aina ya Fibre yenye rangi nyeupe na bluu isiyokuwa na usajili ikiwa na injini ya Yamaha HP 15, Chupa za Hewa ya Oxygen 02, (Diving Cylinder) na mipira ya kupumulia 02 (regulator).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Almachius Mchunguzi.

Vitu vingine vilivyokutwa ni Tega ya kuokotea Samaki, Kiberiti kimoja na Samaki aina mbalimbali Kilogramu 30 waliovuliwa kwa kutumia baruti, ambao walithibitishwa na Afisa Uvuvi kuwa hawafai kwa matumizi ya Binadamu huku upelelezi ukiendelea ili kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa.

Kuhusu Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha maafa na uharibifu wa miundombinu kwa Wananchi, Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kiusalama, ikiwa ni pamoja na kuongeza umakini kwa kujali usalama wao pale wanapokuwa kwenye shughuli mbalimbali pindi mvua zinaponyesha.

Kagere atoa ufafanuzi ushangiliaji wake
Idadi Wanawake waliofanyiwa ukatili wa kijinsia yatisha