Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema juhudi za uokoaji katika ajali ya Ndege iliyotokea Ziwa Victoria zinaendelea kufanywa na Jeshi la Zimamoto na Jeshi la Wananchi (WTZ), kwa kushirikiana na Wavuvi.
Kamananda Mwampaghale amesema, Ndege hiyo ya Precision Air imeanguka ndani ya Ziwa Victoria asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 baada ya kushindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba na kusema kwasasa wanaendelea na zoezi la uokoaji na taarifa kamili ataitoa baadaye.