Treni mbili za abiria zimegongana nchini Pakistan mapema leo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30, huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP Afisa wa shirika la reli nchini Pakistan, tamesema reni hiyo ambayo ilikuwa ikitokea Karachi iliaacha njia karibu na eneo la Daharki, kaskazini mwa mkoa wa Sindh, kabla ya kugongana uso kwa uso na treni nyingine.
Umar Tufail, afisa wa polisi katika eneo la Daharki, ameripoti idadi ya awali ya vifo 30 katika ajali hiyo.
“Watu kadhaa wamefariki dunia na wengine wengi bado wamekwama ndani ya treni,”
Mamlaka za reli zimesema zimeagiza uchunguzi wa ajali hiyo wakati shughuli za uokoaji zikiendelea.
Matukio ya ajali nchini Pakistan ni ya kawaida wakati serikali ikishindwa kuboresha miundombinu ya treni ambayo ipo katika hali mbaya.
Itakumbukwa mwaka 1990, treni ya abiria ilitoka nje ya njia na kuigonga treni ya mizigo, na kusababisha vifo vya watu 210, katika ajali mbaya zaidi kutokea katika historia ya Pakistan.