Aliyekua mkaguzi wa chakula cha Rais Mzee Abdalah Chasamba amesimulia tukio la kwanza kutokea la kiusalama baada ya uhuru, pindi Hayati Mwalimu Julius Kambarege Nyerere akiwa nchini Malawi kwa Rais wa Nchi hiyo, Samora Machel ambapo walifanikiwa kulidhibiti.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media katika kipindi maalumu kinachowakutanisha wanasiasa, watunga sera na watu mashuhuri walioweka historia Tanzania.

Mzee Chasamba alisema, Ikulu ya Malawi kwa kipindi hicho ilikuwa mlimani na ulinzi kwa wakati ule haukuwa kama wa wakati huu kutokana nchi za Afrika zilikuwa zimeanza kupata Uhuru.

“Ikulu ya Malawi ni kama ipo mlimani sana na kwa chini kidogo kulikuwa na majani ambayo si makubwa sana, na ulinzi ulikuwa umeimarishwa lakini kwa upande wa bondeni hawakuimarisha ulinzi sana waliacha wazi na askari walikaa maeneo ya karibu na Ikulu,” amesema

“tukiwa tumekaa nje sisi tulikuwa pembeni na marais tunachungulia huku na huku na pale nilipokaa nilikuwa peke yangu na askari wengine walikuwa pembeni kidogo mimi nilikuwa karibu na Rais Nyerere”.

Kwa mbali mara namuona kijana upande wa bondeni anatambaa halafu ananyanyuka ana kuja usawa wa marais walipo, mara ya kwanza mara ya pili namuona anasogea tuu nikwambia yule askari mmoja angalia kule kuna mtu anakuja anatambaa,” amesimulia Chasamba

“Na sisi tukatambaa usawa wa yule kijana kabla hajafanya tukio tulimuwahi na kumwambia annyue mikono juu baada ya kumsachi tulimkuta na bastola, tulimnyanganya na yeye mwemyewe akachukuliwa na askari wa kule wakampeleka Polisi,” amesema Chasamba

Twaha Kiduku: Ninaogopa Sindano kuliko ngumi ya mpinzani
Watoto waliopanda mlima siku saba wapelekwa mashujaa