Kiungo kutoka nchini Ghana na Klabu ya Azam FC, James Akaminko ameikataa nafasi ya tatu ambayo timu yake imeshika kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii huku akisema wanarudi kama mbogo kwenye Ligi Kuu Bara.

Akaminko amesema Azam FC kushika nafasi ya tatu sio hadhi yao, ingawa wanakubaliana na matokeo na kwamba wamezitumia mechi hizo kuwajenga kwa kuwa bora zaidi Ligi Kuu Bara.

Akaminko amesema wachezaji na makocha wameumizwa na matokeo ya kumaliza nafasi ya tatu na sasa wanataka kuhakikisha wanapoanza mikikimikiki ya Ligi Kuu hawaingii kushiriki, bali kushindania taji.

“Tunakubaliana na hiki kilichotokea kwa kuwa ndicho Mungu ametupangia, lakini hatujafurahia. Hii sio nafasi yernye hadhi kwa Azam FC. Tumetumia mechi hizi kama elimu ya kujifunza na kujipanga.” amesema Akaminko.

“Huko kwenye ligi hatutataka kuruhusu mambo kama haya. Tutakuja na nguvu kubwa ili tuchukue kombe na hatutaingia kama washiriki, tunakuja kushindana.”

Katika mechi mbili za mashindano hayo Azam FC ilipoteza mabao 2-0 dhidi ya Young Afrians kisha ikaifunga Singida Fountain Gate mabao kama hayo mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Mtibwa Sugar waitambia Simba SC Morogoro
Hatimaye ECOWAS wakubaliana jambo kuhusu Niger