Msafara wa watu 50 wakiwemo Wachezaji na Benchi la Ufundi la Al Ahly ya Misri unatarajiwa kutua nchini kesho Alhamisi (Novemba 30) tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi (Desemba 02) dhidi ya Young Africans katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Young Africans watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo huo wa Mzunguuko wa Pili wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, utakaoanza majira ya saa nne usiku.
Ikumbukwe Young Africans ilipoteza mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kundi D, kwa kufungwa mabao 3-0 ugenini dhidi ya CR Belouizdad ya nchini Algeria huku Al Ahly ikishinda 3-0 mbele ya, Madeama FC ya Ghana.
Taarifa kutokana nchini Misri zimeeleza kuwa Msafara wa klabu ya Al Ahly unatarajiwa kuwa na jumla ya watu 50 wakiwa ni Wachezji, Benchi la Ufundi na Viongozi.
Jumla ya watu 50 watatua Alhamisi wakiwa ni Wachezaji, Benchi la Ufundi na Viongozi wa A Ahly ambapo watakuwa na siku mbili za kufanya mazoezi kwa maana ya Alhamisi jioni na ljumaa kisha Jumamosi watacheza na Young Africans.
Lakini ukiachana na watu hao 50 watakaofika Alhamisi kuna baadhi ya viongozi kama watatu tayari walishatangulia nchini Tanzania kwa ajili ya kuweka mazingira sawa kabla ya ujio wa timu nzima, kimeeleza chanzo hicho.