Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa imetoa kibali kwa makampuni ya Simu nchini kusajili upya kadi za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.
Ambapo usajili wa laini za simu kwa alama za vidole zitaanza kutumika kuanzia februari 5, 2018.
Hayo yamesemwa na kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa (TCRA), Semu Mwakyanjala na kuwatoa hofu wananchi kwamba tayari walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.
”Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi” amesem Mwakyanjala.
Amefafanua kuwa mfumo huo utatumia zaidi alama za kidole na picha ni wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.