Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amekiri kuwa ni kweli serikali ya Tanzania inadaiwa na viwanda vya ndani huku akisema kuwa wanaosababisha deni lisilipwe ni watanzania wasiolipa kodi.

Ameyasema hayo hii leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza kwenye wizara yake ambapo aliulizwa kuhusu mkakati wa serikali kulipa madeni hayo ili kuweza kunusuru anguko la viwanda ambavyo vimeanzishwa kwa nia njema.

“Kwa niaba ya serikali nasema ndio serikali inadaiwa na sasa tunaongeza jitihada za kuhakikisha kwamba kila stahili ya serikali inakusanywa na kile kitakachokusanywa ndicho tutakachowalipa wale,”amesema Mwijage

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali haijawalipa kwa sababu na wao hawajalipwa na kuna baadhi ya watu ambao hawapendi kulipa kodi.

 

Alama za vidole sasa kusajili laini za simu
Nembo ya umoja wa wanamitindo yazinduliwa