Kwa zaidi ya wiki tatu sasa, mwanamuziki Rich Mavoko amekuwa akipaza sauti za kuunadi ujio wa album yake mpya aliyopanga kuiachia rasmi Machi 18, 2022.

Licha ya mashabaiki na wadau wa muziki wa Mavoko kuisubiri kwa hamu album hiyo, mapema leo Machi 17, Mavoko ameutumia ukurasa wake wa mtadao wa Instagram kuchapisha taarifa za kusogeza mbele zoezi la kuachia album hiyo.

Mavoko amedai kuwa hiyo ni kupisha kipindi cha maombolezo ya kumbukizi za kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

“Album ya FUNDI ilitakiwa itoke Tarehe 18 Machi, lakini ni vyema zaidi kuchukua siku hizi kuyakumbuka yale makubwa na ya kihistoria yaliofanyika na mpendwa wetu Dkt John Pombe Magufuli. Aligusa maisha ya wengi na wengi bado tunamkumbuka. Hatuna budi kushukuru na kuendelea kumuombea amani popote alipo!, FUNDI itakufikia popote ulipo tarehe 25 March 2022,” ameandika Mavoko.

Mavoko amebainisha hilo muda mfupi tangu alipochapisha ujumbe mwingine wenye lengo la kuwashukuru mashabiki kwa kumshika mkono wakati wote ambao amekuwa kwenye muziki huku akilitambulisha rasmi jina la album hiyo.

“Imekuwa safari ndefu ya kupanda na kushuka kufikia hapa. Nawashukuru sana kwa support endelevu mnayonipa na kwa upendo mnanionyesha kiasi cha kuniheshimisha kama MESSI na FUNDI wa Bongo Fleva, FUNDI hili ndio jina rasmi la album yetu mpya.  Are you ready?” Aliandika.

Wananchi wa Chato waomba kujengwa sanamu la Magufuli
Serikali imedhamiria kuondoa uzembe, rushwa mahala pa kazi