Wananchi wilayani Chato mkoani Geita, wameiomba serikali kuwajengea sanamu la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, hayati Dk. John Magufuli.

Wmetoa ombili hilo wakati wa hafla ya kumbukizi ya kifo cha Hayati Magufuli Mchi 17, 2022 katika uwanja wa Magufuli uliopo mjini Chato mkoani humo.

Naye mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Samuel Bigambo, amesema wanaamini uwepo wa sanamu la kiongozi huyo shupavu litaweka alama isiyofutika kwa vizazi vijavyo.

“Sisi wananchi wa Chato, tulikuwa tunaomba kwanza mkoa, tulishaomba na michakato inaendelea na tunaamini Rais wetu Samia Suluhu Hassan analifanyia kazi” amesema Bigambo.

Aidha ameomba kuwa sanamu la Hayati Magufuli lijengwe kwa njia panda ya kuingia katikati ya mji au lijengwe katika uwanja uliopewa jina la Magufuli.

“ Ikiwekwa sanamu, tutakapokuwa tunapita tunamuona na hata vizazi vitakavyokuja baada yetu, vifike vione kwamba huyu ndiye hayati John Pombe Magufuli, aliyefanya mambo makubwa Tanzania,” amesema .

Naye mkazi wa Kata ya Muungano (Kata ya Magufuli), Esther Kilole, amesema sanamu la hayati Dk.Magufuli likijengwa kwenye mtaa na kata aliyokuwa anaishi, itakuwa ni alama ya kudumu.

Afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka mwanafunzi mara bili
Album ya Mavoko yasitishwa