Wakati Tanzania ikiadhimisha mwaka mmoja tangu kufariki kwa Aliyekuwa Rais wa Nchi John Pombe Magufuli, mgombea urais wa Kenya Raila Odinga ameweka wazi kuwa alikuwa mshauri wa Hayati Magufuli katika uongozi wake kabla ya kufikwa na umauti.

Akizungumza na Shirika la habari la BBC, Raila ameeleza kuwa utaratibu aliotumiwa na marehemu John Magufuli kuibadilisha Tanzania ulikuwa ni mkakati wake kuhusiana na mianya ya ufisadi.

Ikumbukwe pia wakati akizungumza katika kaunti ya Migori mnamo Desemba 2021, Raila alisema ndiye aliyemsaidia Magufuli kutambua ufisadi ambao ulikita mizizi katika tawala zilizopita nchini Tanzania na ambao ulihitaji kushughulikiwa ili taifa la Tanzania liweze kukua kiuchumi.

“Nilikuwa mshauri wa Magufuli na alikuwa akinipigia simu saa 12 asubuhi kuniuliza kuhusu masuala mbalimbali, Nilimwambia ni wapi angeweza kupata pesa, Nilikaa naye kwa muda wa wiki moja alipochaguliwa. Nilimweleza mianya ya kuziba ili kumsaidia kuzalisha pesa kwa nchi.

Enzi za uhai wake Dkt John Pombe Magufuli aliwahakikishia watu wa Muheza kuwa hatabadilika huku akisisitiza kuwa atalala mbele na mafisadi na kuwatumbua kikamilifu.

Aliyasema hayo March 3, 2017 akiwa katika ziara mjini Tanga wakati akihutubia wananchi wa Muheza. “Wanamuheza na Watanzania kwa ujumla waliamua kwamba Rais atakuwa Magufuli na mimi baada ya kuteuliwa kuwa Rais nataka niwahakikishie sitabadilika nitalala mbele na haya mafisadi nitayatumbua mpaka yatumbuke kikamilifu, sitaangalia sura zao, sitaangalia utajiri wao nitakachoangalia ni maslahi ya Watanzania masikini ambao wameteseka kwa muda mrefu.

Hayati John Pombe Magufuli alipatwa na matatizo ya moyo Machi, 2021, miezi michache baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa Tanzania kwa awamu ya pili baada ya kumaliza awamu yake ya kwanza ya Urais iliyodumu miaka 5 kuanzia 2015 hadi 2020.

Kenya:Odinga amtaka Uhuru atakapokua Rais
Serikali yazindua mfumo wa utoaji kibali kwa wasanii kidigitali