Mlinda Lango kutoka nchini Uganda, Ali Ramathan Mwirusi amekamilisha uhamisho wa kudumu kwenda Hispania katika klabu ya Villajoyosa Sports Club.

Kipa huyo wa zamani wa Mamlaka wa Jiji la Kampala (KCCA) alisaini mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo.

Mwirusi anaungana na Mganda mwingine, George Isiagi aliyejiunga na timu hiyo inayofundishwa na kocha Jose Soler Moya.

Machi mwaka huu, Mwirusi pamoja na beki Simon Baligeya walikaribishwa kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu hiyo ya Villajoyosa Sports Club.

Mapema mwaka 2022, Mwirusi pia alikuwa akifanya majaribio nchini Ufaransa katika klabu ya FC Vaulz En-Velin.

Ikiwa na maskani yake katika mji wa Vila Joiosa, katika Jiji la Valencia, Villajoyosa Sports Club ilianzishwa mwaka 1942 (na inacheza mechi zake za nyumbani katika uwanja wenye kuchu- kua watazamaji 4,000 wa Nou Pla, Vila Joiosa).

Baada ya mechi za maonesho, baadhi ya klabu kutoka nchi za Hispania, Ureno na Ufaransa zilichagua wachezaji 14 wakiwamo Eric Ssenjobe, Rashid Mukungu, Raymond Derrick Onyai, Nicholas Kabonge, Alfred Onek na Ivan Junior Ocholit kuchezea timu zao.

Wachezaji wengine ni pamoja na Andrew Okiring Isiagi, Simon Balageya, Ivan Irinimbabazi, Hakim Kiwanuka, Enock Walusimbi, Sadat Happy Anaku pamoja na makipa Derrick Emukule na Ali Ramathan Mwirusi.

Mshambuliaji wa zamani wa KCCA, Sadat Happy Anaku alipata mkataba na klabu ya Scotland ya Dundee United.

Beki Enock Walusimbi ambaye alikuwa nahodha wa zamani wa klabu ya Express, yeye alisajiliwa na klabu ya Peterhead Football ambayo pia ni ya Scotland.

Othman ataja fursa ukuzaji wa Uchumi, maendeleo
Serikali imefanyia tafiti Teknolojia mbadala wa Zebaki