Mtu mmoja aliyefanyiwa upasuaji wa ubongo kimakosa nchini Kenya ameruhusiwa kuondoka hospitalini hapo na kuzungumzia yaliyompata.
Samwel Kimani amesema kuwa alikuwa amepoteza fahamu wakati alipokuwa hospitalini hapo na hakufahamu kilichosababisha madaktari kumfanyia upasuaji.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo cha televisheni ya NTV, ambapo amesema kuwa hakustahili kufanyiwa upasuaji huo.
Aidha, kufuatia tukio hilo, Hospitali ya Kenyatta iliomba msamaha baada ya kukiri kuwa vifaa vya kutambua wagonjwa hao wawili vilikuwa vimechanganyika.
Hata hivyo, tukio hilo lilisababisha kupewa likizo ya lazima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Lilly Koros ili kupisha uchunguzi.