Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Urusi wako ziarani barani Afrika huku kukiwa na taarifa kuwa mawaziri hao Rex Tillerson wa Marekani na  Sergey Lavrov wa Urusi wanaweza kukutana ingawa Marekani imekanusha taarifa hizo.

Urusi imesema kuwa Tillerson na Lavrov wote wanakaa katika hoteli ya kifahari ya Sheraton mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo Alhamis Tillerson atakuwa anakutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia anayeondoka madarakani.

Aidha, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Heather Nauert alisema wiki hii kwamba Marekani haijapokea ombi lolote la mkutano na Tillerson kutoka kwa serikali ya Urusi na kwamba haikuwa na tangazo lolote la mkutano huo.

Hata hivyo, ubalozi wa Urusi nchini Marekani umeilaumu Marekani kwa kusema kuwa haijatuma maombi ya kukutana na Tillerson.

 

Makamu wa rais awahimiza wanawake kuchangia maendeleo
Wanawake zaidi ya 500 wauzwa Uarabuni