Shirika la kutetea haki za binaadamu nchini Burundi (ONLCT) limesema kuwa zaidi ya wanawake 500 kutoka nchini humo wameuzwa katika nchi za kiarabu ikiwa ni pamoja na Oman, Saudi Arabia, Kuwait na Lebanon

Uchugunzi uliofanywa na shirika hilo umebaini kuwa wasimamizi wa mtandao huo wanapokea kiasi cha dola elfu moja kwa kila mwanamke au kwa kila msichana.

Aidha, Shirika hilo limeitaka serikali ya Burundi kupambana na maovu hayo ya kuuzwa kinamama na wasichana na kusafirishwa katika nchi za kiarabu.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo la ONLCT, ameongeza kuwa wanawake na wasichana 527 ndio waliouzwa katika biashara hiyo mwaka jana.

 

Tillerson na Lavrov wazidi kukwepana
Kikosi kazi Taifa Stars mchezo dhidi ya DRC na Algeria chatajwa