Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga mapema leo ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya shirikisho la soka duniani, FIFA.

Taifa stars inatarajia kucheza michezo hiyo mwezi huu, ikianzia ugenini nchini Algeria Machi 22 dhidi ya mwenyeji wao, kabla ya kurejea nyumbani kucheza na timu ya taifa ya DR Congo machi 27 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa ni pamoja na magoli kipa, Aishi Manula, Abdukrahman Mohamed na Ramadhani Kabwili, katika nafasi ya ulinzi Mayanga amemjumuisha Shomari Kapombe, Hassani Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Abdi Banda na Erasto Nyoni.

Viungo walioitwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na Hamis Abdallah, Mudathir Yahaya, Said Ndemla, Faisal Salum, Abdulazizi Makame, Farid Musa, Thomas Ulimwengu, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya na Mohamed Issa.

Washambuliaji waliopo kwenye kikosi hiko ni pamoja na Mbwana Samatta, Saimon Msuva, John Bocco n Yahaya Zayd.

Kwasasa Tanzania inashika nafasi ya 146 kwenye viwango vya FIFA, Wakati DRC ipo katika nafasi ya 39 na Algeria inakamata nafasi ya 63.

Wanawake zaidi ya 500 wauzwa Uarabuni
JPM awapongeza wanawake wote