Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 8, 2018 katika siku ya wanawake duniani amewapongeza wanawake wote wa Tanzania na kuwatakia kheri katika siku yao muhimu.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli ametoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kuwa wanawake wamekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii na kusema daima ataendelea kuwaheshimu.

“Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Kikosi kazi Taifa Stars mchezo dhidi ya DRC na Algeria chatajwa
Mwanamichezo ashambuliwa kwa msumeno