Naibu Waziri  wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amewataka waajiri kuhakikisha wanatoa mikataba kwa vibarua wanao wapa kazi hata kama ni kazi za muda ili kuondoa msuguano baina ya viwanda na vibarua hao.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya viwanda Jijini Dar es saam na kukutana na malalamiko kutoka kwa vibarua hao na wafanyakazi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa imekua ni hali ya kawaida kwa baadhi ya wamiliki wa viwanda na kampuni kushindwa kutoa mikataba ya kazi kwa vibarua na wafanyakazi wao hali ambayo serikali imekataa hali hiyo na kuagiza utoaji wa mikataba ili kuwalinda wafanyakazi.

Nondo apatikana akiwa hai Mafinga
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 8, 2018