Desmond Ricks, Mkaazi wa Detroit Marekani ambaye amesota miaka 25 jela kwa kosa la mauaji kutokana na ushahidi wa kutungwa amefungua kesi mahakamani akidai kulipwa zaidi ya dola za Kimarekani milioni 125, ambayo ni mabilioni ya shilingi za Kitanzania.
Ricks alifunguwa jela miaka 32 mwaka 1992 kwa madai kuwa alimuua rafiki yake, Gerry Bennett kwa kumpiga risasi nje ya mgahawa mmoja.
Jaji wa Mahakama ya Juu amefanya mapitio ya rufaa iliyowasilishwa na mwanasheria wa Ricks na kubaini kuwa ushahidi uliotumika kumtia hatiani ulitengenezwa.
Uchunguzi wa ziada umebaini kuwa risasi zilizotolewa kwenye mwili wa marehemu hazikuwa zinaendana na bunduki ambayo iliwasilishwa kama kifaa kilichotumika kwenye mauaji hayo.
Rick ambaye anasaidiwa na mwanasheria wake, Wolfgang Mueller anawashtaki maafisa wa ngazi za juu wa polisi ambao waliwasilisha ushahidi huo pamoja na aliyekuwa anahusika na upelelezi wa kesi yake, Donald Stawiasz.
- Madaktari mbaroni kwa biashara ya viungo vya binadamu
- Meya: Madiwani wa Chadema waliojiuzulu wanaomba kurudi
Inaelezwa kuwa bunduki iliyowasilishwa kwenye ushahidi ni ya mama yake Ricks lakini haina uhusiano wowote na risasi zilizokutwa kwenye mwili wa marehemu.
“Nilikuwa katika eneo tofauti na kwa wakati tofauti. Sikuwa nahusika kwa lolote na hili. Walinitengenezea na kufyatua risasi kutoka kwangu,” Ricks ameeleza.
Kwa mujibu wa sheria ya Michigan, mtu aliyehukumiwa kwa kosa ambalo hakulifanya anatakiwa kulipwa fidia ya $50,000 kwa kila mwaka mmoja aliokaa jela.