Fareed ‘Fid Q’ Kubanda amejipanga kufanya jaribio kubwa la kuwapatanisha mafahari wawili wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Diamond ambao hivi karibuni wamewasha tena moto mkubwa wa ‘bifu’ lao.

Fid ameweka wazi mpango wake huo ikiwa ni siku chache baada ya Diamond kutumia wimbo wake mpya ‘Fresh’ kufanya remix ambayo ndani yake alirusha makombora kwa Ali Kiba mara mbili.

Rapa huyo nguli amesema kuwa mvutano wa kiushindani kwenye muziki huchangamsha muziki lakini unapofika mbali na kuhusisha maisha binafsi unaweza kuwa hatari na kuleta madhara, hivyo unapaswa kukemewa.

“Nafikiria kuwakutanisha hao wote wawili tuone kama wanaweza kumaliza tofauti zao, kwasababu wote wawili mimi nipo nao sawa,” Fid ameiambia Clouds TV.

Diamond na Ali Kiba wamekuwa katika hali ya kutoelewana kwa muda mrefu ingawa mara kadhaa walisikika wakieleza kuwa hawana tofauti na kila mmoja kumuombea kura mwenzake kwenye tuzo za kimataifa.

Hata hivyo, kauli zao hugeuka kuwa maneno ya mpaka rangi upepo hususan wiki hii waliposhambuliana.

Diamond alirusha makombora yake kwenye mshairi ya ‘Fresh Remix’ akirap lakini Ali Kiba alirusha majibu ya makombora yakee kupitia mtandao wa Twitter. Ugomvi huo pia uliomhusisha mwanafamilia mpya wa RockStar4000, Ommy Dimpoz ambaye alifika mbali kupitia instagram.

Leo Ali Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya aliouita ‘Seduce Me’.

RC Makalla awapiga kitanzi wakurugenzi Mbeya
Aliyefungwa jela Miaka 25 kwa mauaji ya kusingiziwa adai mabilioni