Mtu mmoja raia wa Iran, Mehran Karimi Nasseri ambaye amekuwa akiishi katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle jijini Paris kwa miaka 18, amefariki dunia kwa mshituko wa moyo.

Nasseri, ambaye amefariki hapo jana Novemba 12, 2022 aliishi katika uwanja huo wa ndege kutoka mwaka 1988 baada ya kukosa hati za ukaazi na aliondoka Iran kwenda masomoni Uingereza mwaka 1974 na aliporudi alidai kufungwa kwa kumpinga Mfalme na kisha alifukuzwa bila ya pasipoti.

Raia wa Iran, Marehemu Mehran Karimi Nasseri, aliyeishi uwanja wa ndege kwa miaka 18. Picha ya Quizmaster Trivia.

Kisa chake, kinaonesha kuwa aliomba hifadhi ya kisiasa katika nchi kadhaa barani Ulaya na baadaye Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, nchini Ubelgiji lilimpatia nyaraka za ukimbizi ambazo hata hivyo ziliibwa akiwa jijini Paris.

Kufuatia kadhia hiyo, Nasseri alikamatwa na Polisi wa Ufaransa lakini hawakuweza kumfukuza nchini humo kutokana na kutokuwa na hati rasmi za utambulisho wake na hadithi yake ikachangia utengenezaji wa filamu ya “The Terminal”.

Operesheni M23: Kikosi cha Kenya chawasili DRC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 13, 2022